Sekta ya Uchimbaji Madini Nchini na Ulipaji Kodi ya Mapato

Sekta ya Uchimbaji Madini Nchini na Ulipaji Kodi ya Mapato

Chemba ya Madini na Nishati (TCME) imetambua na kuguswa na taarifa zisizo sahihi kwamba kampuni zinazojihusisha na uchimbaji mkubwa wa madini zimekuwa zikifanya shughuli zake hapa nchinibilayakulipakodiyamapato.Chembahiinimuwakilishi wa makampuni wanachama waliorasimisha shughuli zao katika sekta ya madini kuanzia kampuni ndogo za utafiti wa madini hadi wachimbaji wakubwa na wa kati wa madini, pamoja na makampuni yanayotoa huduma kwa makampuni yanayofanyautafiti na uchimbaji wa madini. Chemba na wanachama wake wanaunga mkono uwepo wa sekta ya uchimbaji madini inayoratibiwa vema na inaweka msisitizo mkubwa katika kuhakikisha shughuli za wanachama wake zinaendeshwa kwa kufuata sheria nakanuni zilizowekwa na mamlaka za Serikali hapa nchini.

Makampuni ya uchimbaji madini hapa nchini yanaratibiwa kwa kiwango cha juunamamlakazilizochiniyaSerikaliilikuhakikishayanafanyashughuli zake kwa kufuata sheria na kanuni za nchi. Makampunihayayameendeleakuchangiakwa kiasi kikubwa uchumi wa nchikwanjiambalimbaliikiwemoutengenezaji wa ajira pamoja na ulipaji wa kodi. Katikaripotiyautendaji ya mwaka 2015 ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ambao wanafanya kazi chini ya Wizara ya Nishati na Madini, imeripotiwa kwamba makampuni makubwa ya uchimbaji madini hapa nchini, kwa ujumla wake, kati ya mwaka 2009 na 2015 yamewezakulipakwaSerikalizaidiyaShilingi Bilioni 870 (USD390 Milioni) kama mrabaha, na zaidi ya Shilingi Bilioni 680 (USD305 Milioni) kama kodi ya mapato, hii ni mbali na kodi nyingine zisizo za moja kwa moja ambazo pia zimelipwa.

Katika mwaka wa 2015 pekee, migodi mitano mikubwa ya uchimbaji Dhahabu pamoja na mgodi mmoja wa kuchimba Almasi, kwa pamojailiwezakulipakwaSerikalizaidiyaShilingi Bilioni 146 (USD65.5 Milioni) kama mrabaha na zaidi ya Shilingi Bilioni 380 (USD170 Milioni) kama kodi nyingine ikiwamo kodi ya mapato. Viwangohivinidhahiri vitakuwa vimeongezeka zaidi kwa mwaka 2016.

Zimekuwepo pia taarifa kwamba makampuni haya ya uchimbaji mkubwa wa madini yamekuwa yakifaidika kwa kurejeshewa kodi yaongezeko la thamani (VAT) pasipo uhalali wa kupata marejesho hayo. Taarifa hizi si sahihi. Ukweli ni kwamba makampuni ya uchimbaji mkubwa wa madini yamekuwa na yataendelea kusafirisha nje ya nchi kwa ajili ya kuuza madini yote ambayo wanayazalisha hapa nchini. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 (VAT ACT 2014) wafanya biashara ambao mauzo yao yote hufanyika kwakuuzanjeyanchihukadiriwakodiyaongezeko la thamanikwakiwango cha sifuri (zero rated) nakwasababuhiyobasihustahilikurejeshewakodiya VAT ambayo huilipa kupitia manunuzi wanayoyafanya hapa nchini. Marejesho haya yanafanyika kwa uhalali na yanafuata matakwa ya sheria ya VAT. Ni muhimu ikaeleweka kwamba makampuni haya bado yanalipa kodi ya VAT ambayo huwa hairejeshwi iwapo yatafanya manunuzi ya bidhaa ama huduma ambazo kisheria hazistahili marejesho. Kwa mfano makampuni haya yameendelea kulipa bila kurejeshewa kodi ya VAT pale yanapofanya manunuzi hapa nchini ya huduma za chakula kwa wafanyakazi wake pamoja na manunuziyavipurikwaajiliyamagari madogo ambayo ndiyo yaliyo mengi huko migodini. Ikumbukwe kwamba sheria ya VAT ambayo makampuni ya uchimbaji madini yanafanya kazi chini yake ndiyo hiyo hiyo ambayo inatumika pia kwa makampuni katika sekta nyingine za uzalishaji ambazo mauzo yake yote hufanywa kwenda nje yanchi.

Kwa mujibu waripotiya TMAA yamwaka 2015 sektarasmiyauchimbajimadini mkubwa inatoa ajira za moja kwa moja 7,355 na zaidiya3,000 kupitiamakampuniyawakandarasi.Kwa mujibuwatafitizilizofanyikahukonyumaajiramojarasmihuhudumiawatuwengine 11 wasionakazi.Kwa mantikihiyosekta rasmi ya madini inawezesha wastani wa watu 114,000 kuendelea kuishi na kupata huduma za msingi. Kodi zinazolipwa na makampuni ya madini husaidia kufanikisha shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwamo ujenzi wa miundombinu muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Chemba itaendelea kushirikisha taasisi, mamlaka, vyombo mbali mbali vya habari pamoja na jamii kwa ujumla, katika kuboresha uelewa wa wananchi na mamlaka za nchi kuhusu jinsi gani wanachama wake wanatii sheria za nchi kuhusu kulipa kodi na tozo mbali mbali kwa mujibu wa sheria na kanuni. Vile vile tutaendelea kuelimisha jamii kuhusu mchango mkubwa ambao sekta rasmi ya uchimbaji madini hapa nchini imekuwa ikiutoa katika uchumi wa nchi yetu kupitia uwekezaji, ulipaji wa kodi, utengenezaji wa ajira, kuchangia soko la fedha za kigeni, manunuzi ya huduma pamoja na michango ya hiyari (CSR) kwa shughuli mbali mbali za maendeleo ya jamii. Ni jambo la muhimusanakuhakikisha kwamba wadau wa sektahiiwanaelewakwaufasahajinsisektayautafitinauchimbaji wa madini inavyoendeshwa na kisha waiunge mkono ili iendelee kukua na kuchangia zaidi katika pato la taifa.

Ni muhimu ifahamike kwamba pamoja na kuwanamikataba yakisheria (MDA’s) ambayo inatoaunafuu wa tozo na kodi mbalimbali kwa makampuni yanayojishughulisha na uchimbaji mkubwa wa madini, bado makampuni haya yameridhia kutekeleza matakwa kadhaa yaliyoingizwa na kanuni na sheria ya uchimbaji madini ya mwaka 2010 (Mining Act, 2010) ili hali baadhi ya matakwa hayo yanakwenda kinyume na mikataba (MDA’s) ambayo Serikali iliingia na makampuni haya yalipokuja kuwekeza hapa nchini kwa mara ya kwanza na kabla sheria hiyo (Mining Act 2010) haijapitishwa. Kwa mfano badala ya makampuni haya kulipa kiwango kisichozidi dola za kimarekani 200,000 kwa mwaka kwa halmashauri kama ushuru wa huduma, makampuni haya yamekubali kulipa ushuru huo kwa kiwango cha 0.3% ya thamani ya mauzo yote ya madini. Makampuni pia yamekubali kulipa mrabaha kwa kiwango cha 4% badala ya 3% iliyo kwenye mikataba yao.

Kuhusu Sekta ya Madini Tanzania

Historia ya uchimbaji wa madini hapa chini inaanzia enzi za ukoloni wakati wafanyabiashara wazawa na wale wa ki-Arabu walipochimba na kuuza maliasili za nchi hii ikiwemoDhahabu, Shaba, Fedha, ChumanaChumvi.Uchimbaji wa kwanza wa kibiashara wa dhahabu ulifanyika katika eneo linalozunguka ziwa Victoria chini ya utawala wa ki-Jerumani kati ya miaka ya 1890. Kati ya miaka ya 1920 na 1930 miradi kadhaa ya uchimbaji iliendelezwa na wamiliki kutoka Uingereza pamoja na Afrika ya Kusini. Mojawapo ya miradi hiyo ilikuwa mgodi wa Almasi wa Williamson kule Mwadui.

Kufuatia kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, uendeshaji wa sekta ya madini uliwekwa chini ya Serikali na taasisi zake kama vile Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Shirika la Uchimbaji Madini la Taifa (STAMICO). Sera mpya na sheria zilizopitishwa mwishoni mwa miaka ya 1990 ziliwavutia wawekezaji wageni ambao walianzisha migodi mikubwa ya uchimbaji wa dhahabu. Mgodiwa kwanza wa ainahiiulianzauzalishajimweziNovembamwaka1998.Kwa sasahivinchi yetu ina migodi mikubwa mitano ya uchimbaji wa Dhahabu na mgodi mmoja mkubwa wa uchimbaji Almasi. Ipo pia migodi mingine ya Dhahabu na Almasi ya kiwango cha kati pamoja na makampuni kadhaa yanayoendeleza utafiti wa mashapo yenye madini kwa ajili uanzishwaji wa migodi mingine siku zijazo kwa faida ya wadau wote.

Migodi yote mikubwa ya uchimbaji madini iwe ya Dhahabu au madini mengine yoyote ni miradi ambayo huhitaji mitaji mikubwa kuweza kuianzisha nautaalamu wa haliyajuukuiendesha.Kwa mantikihiyomiradihiihuchukuamudamrefukablamuwekezajihajarudishagharamazake za uwekezaji na kuanza kutengeneza faida inayostahili kukatwa kodi ya mapato. Hii haimaanishi kwamba migodi hiiinapatahasaraisipokuwaukwelinikwambakipatokinachozalishwakwawakatihuokinakosasifayakukatwa kodi. Hali hii ni ya kawaida katika ulimwengu wa uchimbaji mkubwa wa madini na Tanzania haiwezi kuiepuka. Majiraambapokampuniitatakiwa kuanza kulipa kodi yamapatoyanawezakupishananamakisioyamudayaliyoonyeshwakwenyeupembuziyakinifu wakati mradi husika unaanza kutokana na sababu mbali mbali ikiwamo kuporomoka kwa bei ya madini husika na kupanda kwa bei ya mali ghafi zinazotumika kwenye uzalishaji. Katikakipindiambachomwekezajihuendeleakurejeshamtaji wake mgodihuendeleakuchangiapato la taifanauchumi wa nchihusikakwakulipakodizisizozamojakwamojakama vile ushuru wa forodha, kodiyazuio, ushuru wa huduma, tozoyakuendelezastadi, (SDL) pamojana PAYE namichangoyahifadhiyajamiiambayopamojanakwambainatozwakwawaajiriwa(nasehemufulanihulipwanamwajiri – kwamichangoyahifadhiyajamii)

michangohiyoisingekuwepokamawafanyakazihawawasingekuwawameajiriwakatikamgodihusika.Vile vilenivema ikaeleweka kwamba hali hii ya kuchelewa kulipa kodi ya mapato hadi pale gharama za uwekezaji wa mwanzo zitakaporudi si pekee kwa kampuni za uchimbaji madini tubali iko hivyo hata katika sekta nyingine za uzalishaji. Tofautipekeenikwamba muda wa kusubiri huwa mrefu zaidi kwa uwekezaji kwenye sekta ya madini kutokana naukwelikwambauwekezaji wa mwanzokwenyeuchimbaji wa madinihuhitajimtajimkubwazaidi.

Chemba itaendelea kushirikiana na kuhamasisha mashauriano na Serikali kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hii ili kuhakikisha zinatatuliwa na kuiwezesha Tanzania kunufaikaipasavyonamaliasilizake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *